SOUWASA YATUNIKIWA TUZO YA HUDUMA BORA KWA WATEJA
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA) imetunukiwa Tuzo ya Utoaji Huduma Bora kwa wateja (Customer Service Exellence Award) katika kipindi cha miaka 3, utoaji wa tuzo hizo umefanywa katika hafla iliyoandaliwa na Wizara ya Maji jijini Arusha.
Katika hafla hiyo, SOUWASA imeibuka mshindi kwa Mamlaka kubwa za maji nchini zenye wateja zaidi ya elfu ishirini (20,000) , ambapo tuzo hii ilikabidhiwa na Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Hamidu Aweso (Mb) ambaye aliipongeza Mamlaka kwa juhudi zake za kuboresha huduma kwa wananchi.
Ushindi huu unaendelea kuiweka SOUWASA katika nafasi ya kuigwa na Mamlaka nyingine za maji nchini kwa utoaji wa huduma bora kwa wateja.







