Back to Top

Utiaji saini wa mkataba wa Mradi wa Maji wa Miji 28

Naibu waziri wa Maji Mhe.Mhandisi Maryprisca  Mahundi(Aliyekaa mebele kiti chukundu cha kwanza kushoto) akifuatiwa na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma kanali Labani Thanas wakishuhudia utiaji wa saini wa ujenzi wa  Mradi wa Miji 28  na mkandarasi wa kampuni ya china.......

Mwenge Wa Uhuru Waridhia Maendeleo Ya Mradi Wa Maji Wa Uviko Pambazuko

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Godfrey Mnzava ameridhia maendeleo ya mradi wa maji wa Uviko uliopo katika eneo la Pambazuko. 

Ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Songea kwa kuongeza ......

Bodi mpya ya Wakurugenzi SOUWASA yatembelea miundombinu.

Wajumbe wa Bodi mpya ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Songea(SOUWASA), wakiongozwa na mwenyekiti wa Bodi hiyo Bi.Rosalia Mwenda (Aliyevaa nguo ya kitenge katikati) pamoja na Menejimenti ya SOUWASA wakitembelea miundombinu......

Huduma za haraka

Unapataje Ankara Yako

➡️ Piga *152*00#

➡️ Chagua namba 6; Maji

➡️ Chagua namba 1; Huduma za maji za pamoja

➡️ Chagua huduma unayotaka

➡️ Ingiza namba ya Account; (A422.... au B422...)

 

SOUWASA Huduma bora kwa wote

Lipa Ankara Yako

Namba Zetu za Bure

➡️ 0800 110010

➡️ 0677 091360

Mitandao Yetu Ya Kijamii

➡️ Facebook

➡️ Instagram

➡️ Youtube

➡️ Twitter

 

Maunganisho Mapya

➡️ Mteja  kufika katika ofisi za SOUWASA akiwa na passport size mbili pamoja kopi ya hati ya kiwanja,nyumba au kopi ya leseni ya makazi au office.

➡️ Au kufika na picha(Passport size) mbili pamoja na barua ya utambulisho kutoka kwa mwenyekiti wa mtaa au mtendaji iwapo hana hati au leseni ya makazi.

➡️ Ujazaji wa fomu ambayo itahitaji majina matatu ya mteja,namba ya simu pamoja na mtaa ambao eneo lake analotokea mteja.

➡️ Baada ya ukamilishaji wa fomu mteja ataenda kupimiwa eneo lake ndani ya siku saba toka alipo wasiliasha maombi ili kupata gharama halisi.

➡️ Mteja atapatiwa gharama za maunganisho kupitia SMS pamoja na kumbukumbu namba ya malipo.

➡️ Maunganisho ya maji kufanyika ndani ya siku saba baada ya mteja kufanya malipo husika.

➡️ Mteja kukabidhiwa maunganisho baada ya kukamilika.

Taratibu za Kurudisha Maji

➡️ Mteja kulipa deni lote analodaiwa kupitia kumbukumbu namba anazotumiwa ambazo hazibadiliki au kulipa sehemu ya deni mara baada ya makubaliano maalum na ofisi.

➡️ Mteja kufanya malipo ya gharama ya urejeshaji wa huduma(Reconnection Fee) kupitia kumbukumbu namba maalaum kwaajili ya malipo hayo.

➡️ Mteja kusubiri kurejeshewa huduma baada ya kujaziwa fomu maalum ya urejeshaji wa huduma inayoonesha kukamilika kwa malipo husika.

➡️ Huduma itarejeshwa ndani ya masaa 24 ya siku za kazi toka mteja alipofanya malipo.

Bei za Maji 2023/24

Bei za Maji kwa Unit.

➡️Majumbani: 1,680/= Tsh

➡️Taasisi: 1,730/= Tsh

➡️Biashara: 1,770=/ Tsh

➡️Viwanda: 1,770=/ Tsh

➡️Magati/m3: 1,000=/Tsh

➡️Magati/lita 20: 20=/Tsh

 

Ada Maunganisho Mapya.

➡️ 26,000/= Tsh

 

Ada Kurejesha Maji

➡️Majumbani: 28,000/= Tsh

➡️Taasisi: 28,000/=Tsh

➡️Biashara: 28,000/=Tsh

➡️Viwanda: 28,000/=Tsh

 

Tozo za Maji Taka.

➡️Km 0 - 10 (100,000/=Tsh)

➡️Km 10-20 (110,000/=Tsh)

➡️ KM >20 (120,000/= TSh)

 

Tozo maji Taka Huduma.

➡️Majumbani: 480/= Tsh

➡️Taasisi: 780/=Tsh

➡️Biashara: 810/=Tsh

➡️Viwanda: 810/=Tsh