SOUWASA IMEENDELEA KUNG'ARA KWA MWAKA WA PILI MFULULIZO KUSHIKA NAFASI YA PILI MIONGONI MWA MAMLAKA 20 ZA MAJI NCHINI ZENYE WATEJA ZAIDI YA ELFU ISHIRINI.
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA) imeshiriki katika shughuli ya uzinduzi wa taarifa ya utendaji kazi wa Mamlaka za maji nchini kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Taarifa hiyo imezinduliwa na Waziri wa Maji Mhe. Jumaa H. Aweso (mb). Katika taarifa hiyo SOUWASA imeendelea kung’aa kwa mwaka wa pili mfululizo baada ya kushika nafasi ya pili (2) miongoni mwa Mamlaka 20 za maji nchini zenye wateja zaidi ya 20,000.
Tuzo hizo hutolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
Katika tathmini inayofanywa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mamlaka za maji hupimwa kwa kuzingatia vigezo mbalimbali ikiwemo ubora wa huduma kwa wateja, ufanisi wa ukusanyaji wa mapato, upatikanaji wa majisafi na salama, usimamizi madhubuti wa miundombinu ya maji safi na majitaka
Mafanikio haya ni matokeo ya juhudi za pamoja kati ya Bodi ya Wakurugenzi, watumishi wa Mamlaka, ushirikiano wa wananchi, pamoja na uwekezaji unaoendelea katika kuboresha huduma za maji katika Manispaa ya Songea.












