SOUWASA YATUNUKIWA CHETI KWA UTOAJI BORA WA HUDUMA ZA MAJI

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA) imeshika nafasi ya pili katika utoaji bora wa huduma za Maji safi na Usafi wa mazingira kwa Mamlaka kubwa (zenye wateja zaidi ya 20,000). Cheti hiki kimetolewa na EWURA katika uzinduzi wa Taarifa ya Utendaji Kazi wa Mamlaka za Maji kwa mwaka wa fedha 2023/24 pamoja na utoaji wa tuzo kwa Mamlaka zilizofanya vizuri

Tuzo hii ni uthibitisho wa juhudi za SOUWASA katika kuboresha huduma kwa wananchi wa Songea kupitia uwekezaji katika miundombinu na usimamizi bora wa rasilimali.