MWENGE WA UHURU WARIDHIA MAENDELEO YA MRADI WA MAJI WA UVIKO PAMBAZUKO 

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Godfrey Mnzava ameridhia maendeleo ya mradi wa maji wa Uviko uliopo katika eneo la Pambazuko. 

Ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Songea kwa kuongeza idadi ya wananchi wanaohudumiwa na kupitia mradi huo kwa kuwa ndio dhamira kubwa ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo ya maji kichwani.