MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI DUNIANI TAREHE 16-22 Machi, 2024.
Katika kuadhimisha kilele cha Wiki ya Maji Duniani iliyobeba kauli mbiu "Uhakika wa maji kwa amani na utulivu". Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA), leo wameshiriki katika zoezi la upandaji wa miti katika chanzo cha bonde la mto Ruhila.
Zaidi ya miche 500 imepandwa ikiwa ni sehemu ya kuhifadhi chanzo hicho ambacho ni muhimu kwa ajili ya kuwahudumia wakazi wa Manispaa ya Songea.
Katika kuhitimisha zoezi hilo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Jafari Yahaya aliwahimiza watumishi na wananchi kwa ujumla wanaokizunguka chanzo hicho kuendelea kukitunza, kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira na kuzuia shughuli zote za kibinadamu zinazoweza kuathiri utoaji wa huduma ya maji safi.