WATUMISHI WA MAMLAKA WASHIRIKI MAFUNZO YA HUDUMA KWA WATEJA
Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA), wameshiriki mafunzo ya Huduma kwa Wateja yaliyotolewa na Mwezeshaji Bw. Patrick Theodory Mayige kutoka Credit & Debt Master's Co. LTD.
Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka Mhandisi Patrick Kibasa alieleza kuwa mafunzo yamelenga kuwajengea watumishi uwezo, umakini na njia bora za kutoa huduma kwa wateja wake ili kuhakikisha huduma inayotolewa kwa wananchi inawafikia kwa wakati, kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza kipindi wakitoa huduma na kujenga mahusiano mema kati ya mtoa huduma na mpokeaji wa huduma