Back to Top

Muda gani unatumika mpaka mteja kuunganishiwa huduma ya majisafi/taka

➡️Siku saba za kazi baada ya malipo kufanyika

Inachukua muda gani hadi mteja kurejeshewa huduma baada ya malipo?

➡️Ndani ya saa 24 ya siku za kazi

Gharama ya uniti moja ya maji kwa mteja wa majumbani ni Shilingi ngapi?

➡️Shilingi 1680/= kwa uniti moja

Ni taratibu gani mteja anahitaji kufuata ili kuunganishwa na huduma ya majisafi?

➡️Mteja atahitajika kuwasilisha kivuli cha hati ya kiwanja/au offer ya kiwanja/mkataba wa mauziano ya kiwanja/barua ya utambulisho ya wa umiliki wa kiwanja,

➡️Picha mbili za rangi,

➡️Nakala ya kitambulisho cha mpiga kura/ cha taifa au barua ya utambulisho ya m/kiti wa mtaa,

➡️Ndani ya siku saba za kazi kuanzia siku alipo wasilisha taarifa zake, mteja atapokea meseji au kupigiwa siku ikimjulisha gharama zake za maunganisho,

➡️Mteja atahitajika kulipia garama hizo kupitia kumbukumbu namba aliyo patiwa,

➡️Mteja ataunganishiwa maji ndani ya siku saba za kazi toka siku alipo fanya malipo,

➡️Mteja atasomewa dira yake kila mwezi na kupata Ankara kupitia namba ya simu aliyo iwasilisha,

➡️Mteja atahitajika kulipia ankara yake ya maji kila mwezi ndani ya siku 14 toka alipo pata Ankara yake.