MAMLAKA YAKUTANA NA WANANCHI WA BOMBAMBILI SOKOINE 

Wataalam kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA), wamefanya mkutano wa pamoja na wananchi wa Mtaa wa Sokoine kuhusu huduma ya majisafi katika eneo hilo. 

Katika mkutano huo wananchi walipata wasaa wa kuwasilisha changamoto mbalimbali zinazohusu huduma ya majisafi ambapo wataalam wa Mamlaka walizitolea ufafanuzi na kuwasilisha mikakati ya muda mfupi na muda mrefu ya kuboresha huduma ya maji. 

Wananchi walishukuru kwa hatua ambazo zimeanza kuchukuliwa na Mamlaka katika kuhakikisha huduma ya maji inaboreshwa na ushirikishwaji wa wananchi hao katika utatuzi wa changamoto zao.