MENEJIMENTI YAPOKEA TAARIFA YA UTAFITI KUHUSU TATHIMINI YA HUDUMA KWA WATEJA

 

Menejimenti ya SOUWASA, leo imepokea taarifa ya tathmini ya huduma kwa wateja "customer survey satisfaction" kutoka kwa Mtafiti Dkt. Denis Mpagaze wa Chuo Kikuu cha SAUT.


 
Menejimenti ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Patrick Kibasa ilipata fursa ya kupokea taarifa hiyo kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa Mamlaka katika kutoa huduma na kuahidi kufanyia kazi yale yote yaliyowasilishwa kwenye taarifa hiyo ili kuongeza tija na ufanisi wa huduma inayotolewa.