

Naibu waziri wa maji Mhe. Mhandisi Kundo A. Mathew (MB) ameongoza kikao kazi na wataalam wa sekta ya maji mkoa wa Ruvuma
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Kundo A. Mathew, ameongoza kikao kazi na wataalam wa sekta ya Maji Mkoa wa Ruvuma kilicholenga kujadili hali ya utoaji wa huduma ya maji pamoja na mikakati ya kuimarisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma.
Mhe. Naibu Waziri amesisitiza umuhimu wa wataalam wa Maji kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, uwajibikaji ili kuhakikisha wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wanapata huduma bora na endelevu ya maji safi na salama.
Aidha, kikao hicho kimejadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya maji mkoani wa Ruvuma pamoja na kuweka mikakati ya muda mfupi na mrefu ya kuboresha huduma, ikiwemo kukamilisha miradi yote ya maji iliyokwisha anza kabla ya kutangaza miradi mingine.










